TABIA ZA WATOTO NA UTOVU WA NIDHAMU

 


NIDHAMU:

Ni hali ya mtu kuweza kujitawala na kuonyesha tabia zinazokubalika katika jamii. hizi ni baadhi ya tabia za watoto na watu wazima ambazo tunazichukulia kuwa wana utovu wa nidhamu

 

Wanaopenda kusikilizwa (Attention seeking)

Ø Hupenda kudanganya, mizaha kwa wenzao na kwa watu wanaowazidi umri

Ø Hupenda kuvaa vibaya

Ø Hupenda kulia hovyo

Ø Hupenda kupiga kelele hovyo

Ø Hupuuza wajibu wao

Ø Hupenda kuonyesha kuwa wao wanajua zaidi

Kutaka kuonyesha ushawishi, mamlaka (Showing power)

Ø Huwa wakatili

Ø Hupenda kupigana

Ø Wanakuwa wabishi na si watiifu

Ø Hawapendi ushirikiano

Ø Ni wasumbufu na wanapinga kila kitu

Kupenda kulipiza visasi (Revenge)

Ø Hupenda kupigana na kuumiza wengine

Ø Hawaamini juhudi

Ø Hawapendi Kushirikiana na wengine

Ø Huwa na chuki

Kuhisi hajakamilika (Feeling of inadequacy)

Ø Hukata tamaa haraka

Ø Hawaamini katika kuweka juhudi

Ø Hawapendi Kushirikiana na wengine

Ø Hupenda kuzira

Ø Ni rahisi kwao kushiriki katika matumizi ya vileo na dawa zakulevya

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo