Showing posts with label Rika. Show all posts
Showing posts with label Rika. Show all posts

Nawezaje kukabiliana na changamoto za ujana?


Changamoto za ujanani ni nyingi sana kwa kuzungumzia zote ni ngumu lakini kwa sehemu kubwa nyingi zinasababishwa na:

a    Kukosa mwelekeo

Kuna vijana wengi sana ambao hawana mwelekeo wa maisha yao ndio ile ambayo wengi ukiwauliza wanataka kuwa nani wengi wanataka udaktari, urubani na uinjinia ila ukimuuliza hata mmoja wapo wanafanya nini ili wawe hucho wanachokitaka hawajui wafanye nini

Unachotakiwa kufanya hapo ni kujua mwelekeo wako wa maisha, wewe unatakiwa kuwa nani na unatakiwa kufanya nini ukiweza kujua hilo utaweza kuepuka mambo mengi sana yasio na sababu. Ili kujua wewe ni nani

A.    sikiliza yalio moyoni mwako na ufanye jinsi inavyopaswa kufanya. Hii ndio sign ya kwanza kujua wewe ni nani na wala usiogoge hata kama ni kitu ambacho kwenye jamii kinaonekana cha hali ya chini

B.     jua wakati uliopo mfano kwa sasa uko shule basi fanya yanayopaswa kufanywa Shuleni na sio vinginevyo

C.     jua interest zako na zitengee muda maalumu kwaajili ya hizo interest

 

b    Kusimamia msimamo wa maamuzi yako

Ukishajua mwelekeo wako hapo unaweza kuwa na msimamo sababu kila saa unacho cha kufanya. Kosa la kukosa msimamo ni kuwa huna la kufanya kwa hiyo yeyote anaweza kukuambia au kukupa cha kufanya

c    Kuiga watu wengine wanavyofanya

Vijana wengi wanaiga sana watu wengine tunaiga kuvaa, kuongea, kutaka kuimba n.k wewe kuwa wewe kuwa na wewe unataka kuwa nani na katika hilo usiinge wengine. Mfano kila mwanafunzi wanataka kuwa madaktari na hilo wala hana analolijua kuhusu udaktari

Kuwa wa tofauti, jua unachokitaka kisha tumia muda mrefu kujifunza kwa kujifunza utatumia muda mwingi kujiimarisha na muda huo wengine wanatumia kufanya mambo yasio na maana yoyote

 

SWALI: Je nawezaje kuishi na watu vizuri?

 


Kuna vitu vya kuzingatia ili uweze kuishi na watu vizuri

1.       Salamu

Hii ni njia ya kwanza kabisa ya kutaka kuishi na watu vizuri, salimia watu wote awe mdogo au mkubwa, tatizo ni kuwa wengi wetu tunajua kuwa salamu ni kwaajili ya watu wazima.

 

Ngoja nikufundishe kitu hapa:

A.      endapo utakutana na watu wazima wape salamu yao “shikamoo” pia wasalimie kulingana na unavyowaona kama ni baba au mama

B.      Ukikutana na wadogo zako wasalimie kwa kuwauliza “hujambo” kama unawfahamu waite kwa majina au sema “hujambo mdogo wangu”

C.      Kama ukikutana na rika lako pia msalimie “mambo” ama salamu nyingine tu ambayo inaonyesha nyie ni rika moja

 

Kuwataja watu kwa majina au hesima yao kwenye jamii kunawafanya wajihisi furaha na wanahisi kuheshimiwa zaidi

2.       Kujua wanapitia wakati gani

Tambua watu wako kwenye wakati au hali gani na ishi nao kulingana na hali zao: mfano watu wakiwa kwenye sherehe wewe usipige nyimbo za maombolezo nenda furaha nao. Ukikaribishwa mahali fika mapema na kama unahitajika kusaidia saidia, itakusaidia wewe baadae

3.       Shiriki mambo ya jamii:

Shiriki mambo ya Kijamii kama sherehe au misiba, kazi za Kijamii nakadhalika jua kuwa wewe nawe ni binadamu na utawahitaji watu siku ambayo yatakufika

4.       Kuwa mkweli:

sema kweli daima, kama ni ndio na iwe ndio na kama ni hapana iwe hapana kweli kweli. Hii itakusaidia kukuweka kwenye msimamo kwenye jamii. Japo unapaswa kuishi nao vizuri ila usimezwe kwenye jamii. Kuwa mkweli na mwenye msimamo kunasaidia sana hasa wakati wanatafuta mtu mwaminifu

Naamini kwa point hizo nne zimekusaidia, anzia hapo ukipata changamoto nyingine usisite kuwasiliana nasi

Asante

MASWALI MATANO KUHUSU RIKA


Vijana mara nyingine wanaweza kuwa na maswali na mawazo mengi kuhusu suala la umri na jinsi linavyoathiri maisha yao. Hapa kuna maswali matano ambayo kijana anaweza kujiuliza kuhusu suala la umri na mahusiano na watu wa rika lake:
 

  1. "Je, ni muhimu kuwa na marafiki wa rika moja?"

    • Vijana wanaweza kujiuliza umuhimu wa kuwa na marafiki wa rika moja. Wanaweza kutafakari jinsi urafiki na watu wa rika lao unavyoweza kuwa na athari kwenye maendeleo yao ya kijamii na kiakili.
  2. "Ninawezaje kushughulikia tofauti za umri kwenye mahusiano?"

    • Kijana anaweza kujiuliza jinsi ya kushughulikia tofauti za umri katika mahusiano, iwe ni kwenye urafiki au uhusiano wa kimapenzi. Wanaweza kujiuliza jinsi ya kuwasiliana vizuri na watu wa umri tofauti.
  3. "Je, ni muhimu kulinganisha maendeleo yangu na ya wenzangu?"

    • Vijana wanaweza kuwa na shinikizo la kulinganisha maendeleo yao na ya wenzao. Wanaweza kujiuliza kama ni muhimu kufanya hivyo na jinsi ya kuepuka hisia za kutojiendeleza.
  4. "Ni jinsi gani ya kujenga uhusiano mzuri na watu wa rika lao?"

    • Vijana wanaweza kuwa na hamu ya kujenga uhusiano mzuri na watu wa umri wao. Wanaweza kujiuliza jinsi ya kuvutia marafiki wapya na kujenga mahusiano yenye manufaa.
  5. "Je, ni muhimu kufuata matarajio ya kijamii kuhusu umri?"

    • Kijana anaweza kujiuliza kama ni muhimu kufuata matarajio ya kijamii yanayohusiana na umri, kama vile maendeleo ya kielimu, kazi, au mahusiano. Wanaweza kujitafakari kuhusu jinsi wanavyoweza kufuata njia yao wenyewe na kufikia malengo yao.

Maswali haya yanaweza kuwasaidia vijana kuelewa zaidi jinsi umri unavyoathiri maisha yao na kujenga uelewa mzuri wa kujiamini na kuchagua njia zinazolingana na malengo yao binafsi.






 

© all rights reserved
made with by templateszoo