Showing posts with label Family. Show all posts
Showing posts with label Family. Show all posts

KUWA MFANO


Kuamka mapema

Hakikisha wewe ndio wakwanza kuamka kabla ya wengine kwa vijana kuamka mapema ni kama adhabu kwao, kwa hiyo ukiweza kuamka mapema akili zao zitajenga uelewa kuwa kuamka mapema ni swala la Kawaida na sio adhabu. Kama wakiweza kuamka mapema watajifunza kulala mapema hivyo hawatakuwa wakifanya vitu viovu usiku wakati umelala

Kwenda kanisani

Tatizo linalotukuta muda huu ni vijana kutokwenda kanisani na walivyokuwa watoto walikuwa wanaenda Sunday school. Hii ili sababiswa na wazazi wao wakiwa watoto. Unakumbuka wakati ule baba kalala chumbani kwake anawaamsha mwende kanisani? Akitoka chumbani akukute hujaenda kanisani anakuombeza haswa. Kichwani kwa watoto huwa panajengeka kuwa kwenda kanisani ni swala la watoto ila ukifika ukubwani halikuhusu

Kufanya kazi za nyumbani kwa pamoja

Kuna vitu vya msingi kwa watoto kujua moja wapo ni kuwa kazi za nyumbani ni majukumu ya Kawaida ya kila siku na ya lazima, hili unamfundisha mwanao Kutokuwa mvivu. Swala la mwano kujua kufanya usafi kwa mfano, sio baya na hata akiwa na wafanyakazi watakaokuwa wanamfanyia usafi anapaswa kuikaua hiyo kazi kama imefanyika vizuri au la? Atajuaje kama imefanyika vizuri kama hajui kufanya

Kutandika kitanda      

Wengi wetu vitanda vyetu kama vile watu wamefufuka makaburini, ukiamka tandika kitanda mwanao ajifunze utaratibu kuanzia kuamka. Alafu aendelee na kwingine kama kuosha vyombo, kudeki na kukaa kwenye nyumba safi ni raha. sasa kama mwanao hajaanza kutandika kitanda, hataweza kupanga chumba chake, vikimshinda hivyo vya kawaida kuna hatihati hata anaweza kupiga mswaki

Kuwa wa mwisho kupakuwa chakula

Baba yangu alinifundisha kuwa watoto ndio wanakuwa wakwanza kupakuwa chakula, yeye anakuwa wa mwisho. Nikamuuliza kwanini akaniambia watoto ndio wanao hitaji chakula sababu wao Wanakuwa na watu wazima wameshakuwa. Hiki kinaweza kinaweza kumtengenezea mwanao uwajibikaji, upendo, kujituma na kufanya mambo kwaajili ya wengine

 

NJIA MBADALA YA KUZUIA MATUMIZI YA ADHABU ZA KIMWILI

 



1.   Tenga muda wa kukaa na watoto na kuongea nao

2.   Washirikishe watoto katika kufanya maamuzi mbalimbali

3.   Sikiliza na heshima maamuzi ya watoto yasiyo sahihi

4.   Sifia tabia zinazofaa

5.   Endapo upo Umuhimu wa kukosoa ONGEA JUU YA UBAYA WA TENDO HUSIKA NA SIO UBAYA WA MUHUSIKA

6.   Jiweke katika nafasi ya mtoto ili ujue kwann anatenda na kufikiri tofauti

7.   Tengeneza mazingira ya kuwa nao na si kuwa dhidi yao (watoto wakijua kuwa unawajali watahakikisha kuwa wanafanya yale unayowaelekeza ili wasikuangushe)

8.   Pale wanapokuuliza maswali hakikisha unawajibu na sio kuwafukuza maswali yanaweza kuwa yanayoudhi au yasio na maana ila yajibu watoto wanatafuta kuwa karibu na wewe

9.   Wanapofanya makosa wawezeshe kufahamu ni nini wamefanya na maana yake ni nini. Tumia maswali kuwawezeha kutambua makosa yao

10.         Hata kama huvutiwi na matendo yao kamwe usimwonyeshe kuwa humpendi

NJIA BORA ZA KUJENGA NIDHAMU SAHIHI



Hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaaonyesha kuwa matumizi ya fimbo yanarekebisha mtoto moja kwa moja. Wengi walio watu wazima wazazi wao walitumia fimbo kama ndio njia pekee ya adhabu na wengi wetu hatuna tabia nzuri. Kuna tofauti kati ya NIDHAMU na UTII

Nidhamu ni uwezo wa wa kuwa na tabia nzuri mbele ya watu na ukiwa peke yako ila utii ni kutii sharia ya sehemu husika. Wengi wetu hatuna nidhamu tuna utii ndio maana hatuoshi vyombo mbaka tupate mgeni, hatudeki nyumba zetu wala hatutandiki vitanda vyetu.

 

Hizi ni baadhi ya njia bora za kuweza kujenga nidhamu kwa watoto

  1. Kuwapatia watoto njia mbadala na chanya za matendo yasiyofaa:
  2. Kutambua na kuzawadia juhudi na matendo yanayohitajika
  3. Kuwashirikisha  watoto katika kuandaa sharia ndogondogo ili waweze kuzitekeleza kirahisi
  4. Kujihusisha a mambo ya watoto na kuwaheshimu
  5. Kuwa na kauli nzuri wakati wa kuwarudi watoto na kutokuwadhuru kimwili: wachape usiwapige, wachape sehemu sahihi sio kila mahali
  6. Kuwajengea watoto tabia ya kuomba msamaha na kusamehe kwa dhati pale wanapowakosea au kukosewa na wengine
  7. Kutambua na kuendeleza vipaji vya watoto
  8. Watu wazima kuwa mfano wa tabia njema kwa watoto
  9. Kuwawezesha watoto kujifunza kutokana na makosa
  10. Kukemea tabia za watoto na sio watoto

 

© all rights reserved
made with by templateszoo