1. Tenga muda wa kukaa na watoto na kuongea nao
2. Washirikishe watoto katika kufanya maamuzi mbalimbali
3. Sikiliza na heshima maamuzi ya watoto yasiyo sahihi
4. Sifia tabia zinazofaa
5. Endapo upo Umuhimu wa kukosoa ONGEA JUU YA UBAYA WA TENDO HUSIKA NA SIO UBAYA WA MUHUSIKA
6. Jiweke katika nafasi ya mtoto ili ujue kwann anatenda na kufikiri tofauti
7. Tengeneza mazingira ya kuwa nao na si kuwa dhidi yao (watoto wakijua kuwa unawajali watahakikisha kuwa wanafanya yale unayowaelekeza ili wasikuangushe)
8. Pale wanapokuuliza maswali hakikisha unawajibu na sio kuwafukuza maswali yanaweza kuwa yanayoudhi au yasio na maana ila yajibu watoto wanatafuta kuwa karibu na wewe
9. Wanapofanya makosa wawezeshe kufahamu ni nini wamefanya na maana yake ni nini. Tumia maswali kuwawezeha kutambua makosa yao
10. Hata kama huvutiwi na matendo yao kamwe usimwonyeshe kuwa humpendi
No comments
Post a Comment