Nawezaje kukabiliana na changamoto za ujana?


Changamoto za ujanani ni nyingi sana kwa kuzungumzia zote ni ngumu lakini kwa sehemu kubwa nyingi zinasababishwa na:

a    Kukosa mwelekeo

Kuna vijana wengi sana ambao hawana mwelekeo wa maisha yao ndio ile ambayo wengi ukiwauliza wanataka kuwa nani wengi wanataka udaktari, urubani na uinjinia ila ukimuuliza hata mmoja wapo wanafanya nini ili wawe hucho wanachokitaka hawajui wafanye nini

Unachotakiwa kufanya hapo ni kujua mwelekeo wako wa maisha, wewe unatakiwa kuwa nani na unatakiwa kufanya nini ukiweza kujua hilo utaweza kuepuka mambo mengi sana yasio na sababu. Ili kujua wewe ni nani

A.    sikiliza yalio moyoni mwako na ufanye jinsi inavyopaswa kufanya. Hii ndio sign ya kwanza kujua wewe ni nani na wala usiogoge hata kama ni kitu ambacho kwenye jamii kinaonekana cha hali ya chini

B.     jua wakati uliopo mfano kwa sasa uko shule basi fanya yanayopaswa kufanywa Shuleni na sio vinginevyo

C.     jua interest zako na zitengee muda maalumu kwaajili ya hizo interest

 

b    Kusimamia msimamo wa maamuzi yako

Ukishajua mwelekeo wako hapo unaweza kuwa na msimamo sababu kila saa unacho cha kufanya. Kosa la kukosa msimamo ni kuwa huna la kufanya kwa hiyo yeyote anaweza kukuambia au kukupa cha kufanya

c    Kuiga watu wengine wanavyofanya

Vijana wengi wanaiga sana watu wengine tunaiga kuvaa, kuongea, kutaka kuimba n.k wewe kuwa wewe kuwa na wewe unataka kuwa nani na katika hilo usiinge wengine. Mfano kila mwanafunzi wanataka kuwa madaktari na hilo wala hana analolijua kuhusu udaktari

Kuwa wa tofauti, jua unachokitaka kisha tumia muda mrefu kujifunza kwa kujifunza utatumia muda mwingi kujiimarisha na muda huo wengine wanatumia kufanya mambo yasio na maana yoyote

 

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo