Kuna vitu vya kuzingatia ili uweze kuishi na watu vizuri
1. Salamu
Hii ni njia ya kwanza kabisa ya kutaka kuishi na watu vizuri, salimia watu wote awe mdogo au mkubwa, tatizo ni kuwa wengi wetu tunajua kuwa salamu ni kwaajili ya watu wazima.
Ngoja nikufundishe kitu hapa:
A. endapo utakutana na watu wazima wape salamu yao “shikamoo” pia wasalimie kulingana na unavyowaona kama ni baba au mama
B. Ukikutana na wadogo zako wasalimie kwa kuwauliza “hujambo” kama unawfahamu waite kwa majina au sema “hujambo mdogo wangu”
C. Kama ukikutana na rika lako pia msalimie “mambo” ama salamu nyingine tu ambayo inaonyesha nyie ni rika moja
Kuwataja watu kwa majina au hesima yao kwenye jamii kunawafanya wajihisi furaha na wanahisi kuheshimiwa zaidi
2. Kujua wanapitia wakati gani
Tambua watu wako kwenye wakati au hali gani na ishi nao kulingana na hali zao: mfano watu wakiwa kwenye sherehe wewe usipige nyimbo za maombolezo nenda furaha nao. Ukikaribishwa mahali fika mapema na kama unahitajika kusaidia saidia, itakusaidia wewe baadae
3. Shiriki mambo ya jamii:
Shiriki mambo ya Kijamii kama sherehe au misiba, kazi za Kijamii nakadhalika jua kuwa wewe nawe ni binadamu na utawahitaji watu siku ambayo yatakufika
4. Kuwa mkweli:
sema kweli daima, kama ni ndio na iwe ndio na kama ni hapana iwe hapana kweli kweli. Hii itakusaidia kukuweka kwenye msimamo kwenye jamii. Japo unapaswa kuishi nao vizuri ila usimezwe kwenye jamii. Kuwa mkweli na mwenye msimamo kunasaidia sana hasa wakati wanatafuta mtu mwaminifu
Naamini kwa point hizo nne zimekusaidia, anzia hapo ukipata changamoto nyingine usisite kuwasiliana nasi
Asante
No comments
Post a Comment