Ili kukua kutoka kwenye hali yako ya sasa na kuwa mtu unayetamani kuwa, ni muhimu kujijua vyema.
1. Kutambua unapokuwa na tatizo na unahitaji msaada.
2. Kutambua unapokuwa huna jibu.
3. Kuzungumza na mtu unapokuwa hujui la kufanya kuhusu jambo fulani.
4. Kuomba msaada kutoka kwa mwenzako unapohitaji.
5. Kuomba msaada kutoka kwa mlezi unapohitaji.
6. Kuomba msaada kutoka kwa watu katika jamii yako na familia.
7. Kutafuta wataalamu mtandaoni au kupitia uhusiano wako wa kazi kuomba msaada.
Umuhimu wa Kutafuta Msaada
- Hutapambana Pekee Yako:
- Ukishirikisha shida yako umeipunguza nusu ya hiyo shida yako unaposhirikisha changamoto zako na watu wanaoweza kukusaidia, inaongeza nafasi ya kupata suluhisho la shida.
- Unaweza Kujenga Mahusiano Bora:
- Unapopata msaada hasa kutoka kwa watu wenye huruma, kuna uwezekano mkubwa wa kujenga mahusiano na watu hao. Hii itakusaidia kutojihisi pekee tena.
- Ufanisi Wako Shuleni Unaweza Kuimarika:
- Ikiwa shida yako inahusiana na masomo, kutafuta msaada kutoka kwa walimu, marafiki, na hata wazazi wako kunaweza kuongeza uwezekano wako wa kufanya vizuri kitaaluma.
- Inaboresha Ubora wa Maisha ya Kijamii:
- Matatizo hufanya maisha yetu kuwa magumu, hivyo kwa kutafuta njia mbalimbali za kutatua tatizo, unaweza kuongeza nafasi ya kuboresha ubora wa maisha yetu.
No comments
Post a Comment