JINSI YA KUMWAMBIA MTU I KUWA HUMTAKI


Je nawezaje kumwamvia mtu ukweli kwamba simtaki baada ya kunitongoza?

Mimi nitakupa njia amboazo nilishazitumia na nikawaambia watu nao wakazitumia zikafanikiwa

1.       Usijibu chochote:

Ndugu yangu kama mtu anakutafuta kuwa nae kwenye mahusiano huyo atakufata siku zote akitaka “jibu” sasa kwasababu ulishafanya kosa la kumpa nafasi ya kumsikiliza sasa hivi usifanye tena kosa kwa mara ya pili fanya hivi, usimjibu kitu chochote TENA. Nitakupa sababu: endapo utamjibu kuwa humtaki atatafuta maneno mengine ya kutaka kukushahwishi ili tu umkubali na hapo ndio unaongeza mazungumzo ambayo huyataki usijibu la heri wala la shari

 

Endapo atakuwa anatumia simu, basi save hiyo namba jina ambalo ni baya na utalikumbuka mfano ‘msumbufu’ ili atakapopiga usipokee najua akiona hupokei wala hujibu meseji atatafuta njia nyingine ya kukutafuta ikija namba ngeni alafu ukapokea ukajua ni yeye usiikate ila weka pembeni aite “halo” mpaka ache mwenyewe

2.       Mpuuze:

Ili ajue kuwa humtaki kweli mpite usimsalimie, mpuuze haswa. Unaweza msalimia mtu alie pembeni yake alafu yeye ukamwacha hapo fanya hivyo mpaka aombe msamaha na akishaomba msamaha usimwendekeze tema

 

 

Ushauri:

Wakati mtu anakutaka kimapenzi ukweli ni kuwa haikuanzia hapo, ulihsona dalili toka mwanzo kwa mwenendo wake na jinsi anavyokutreat sasa basi ukishaona hizo dalili kimbia wala usikae hapo

 


No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo