1. Kuepuka/kujitoa (avoidance)
· Kujiondoa kwenye mgogoro au kukaa kimya ili kuepusha shari
· Baadhi ya watu hutumia mbinu hii kwa kuogopa kuonekana wakorofi
· Wakati mwingine watu huepuka migogoro ili kujipanga upya
2. Kulazimisha haki yako (forcing)
· Huhakikisha matakwa yao yanatimia hata kama watu wengine wataumia
· Kuhakikisha kwamba wanaweka matakwa yao bayana na kuamua bila kusita
3. Kukubali kupoteza/kuachilia (accommodation)
· Kuhakikisha kwamba matakwa ya wengine yanatimizwa katika migogoro
· Lengo ni kutafuta kupendwa na wengine au kuwatuliza wasijiskie vibaya
4. Kila upande kukubali kupoteza (compromising)
· Kutaka matakwa yao yanatimizwa bila kuharibu mahusiano
· Mbinu hii inahusisha majadiliano ya pande mbili
5. Kushirikiana/kutatua tatizo (problem solving)
· Kuujadili mgogoro kwa kina kwa lengo la kutoa haki kwa kila upande
· Mbinu hii hudumisha mahusiano na pia kuongeza ubunifu wa kunufaika na migogoro
· Mbinu hii huongeza kuaminiana (trust)
Wakati ambapo una lengo la kutatua mgogoro wowote lazima ujue kuwa kila mtu ana upande ambao ana usimamia ambao kwa kila mtu huo ndio ukweli
Aina za ukweli
i. Ukweli wake: hii ni taarifa au msimamo wa mtu ambae mpo nae kwenye mgogoro. Inawezekana akawa haupo sahihi au yupo sahihi
ii. Ukeli wako: huu ni upande ambao wewe unausimamia, unaoamini kuwa ndio ukweli. Inawezekana ukawa haupo sahihi au upo sahihi
iii. Kanuni (objective reality): huu ni upande ambao ni mwongozo wa kanuni kulingana na muktadha wa mahali husika.
Inawezekana mmoja wenu akawa sahihi au wote mkawa sahihi mkawa mmepishana kwenye mtazamo au sababu moja wapo zinazosababisha migogoro. Unaposuluhisha mgogoro usiwe kwenye upande wowote ila simamia kanuni. Tambua kwamba kuna mitazamo miwili kuwa sahihi na kuwa sawa
Sahihi: mfano, mwa mwanafunzi wa darasa la tatu akipewa hesabu hii “5-9” atasema haiwezekani na yupo sahihi
· Usahihi unakuwa kwa wale wa kiwango cha chini
· Kwa baadhi ya mambo ila sio yote
· Huzalisha migogoro mingine baadae
· Kuwe kuna ufatiliaji ili kusizaliwe migogoro mingine
Sawa: hesabu hiyo hiyo mwanafunzi wa darasa la saba akipewa akasema jibu ni “haiwezekani” hatakuwa sahihi ila akitoa jibu ni -4 atakuwa sahihi na ndio sawa
· Hutumika kwa watu waliokomaa akili
· Ndio kweli ilioko haipingiki
· Hakikisha kila upande umeridhia
No comments
Post a Comment