Pamoja na mwamba migogoro inaweza kuwa chanzo cha mabadiliko chanya, isipotatuliwa kwa ufanisi huwa chanzo cha ukosefu wa maendeleo katika jamii
i. Kijamii: migogoro isitatuliwa kikamilifu imekuwa ndio chanzo cha udhaifu katika utoaji wa huduma za kielimu, afya, maji nk. Aidha husababisha kuvunjika kwa ndoa na watoto wasio na malezi sahihi
ii. Kiuchumi: huathiri biashara, miradi, mgawanyo na mapato pamoja na uzalishaji mali
iii. Kisiasa: huathiri maamuzi, uchaguzi, utekelezaji na mipango ya nchi
Mambo sita ambayo mara nyingi ni kiini cha migogoro
i. Taarifa: taarifa kinzani (contradictory information),taarifa ambazao hazijitoshelezi, taarifa zilizofika kwa kuchelewa
ii. Rasilimali: mgawanyo mbaya wa rasilimali kama vile fedha, muda n.k
iii. Changamoto katika mahusiano: jinsi watu wanavyo tegemeana kama kuna upande mmoja ambao hauridhishwi na mambo fulani n.k
iv. Tofauti katika vipaumbele na mahitaji: mahitaji ambayo mara nyingi yanaleta mgogoro ni kutambuliwa (the need for identity) na heshima (the need for respect)
v. Changamoto katika muundo (structure): nani ana mamlaka na anayatumiaje nani anahisi kutengwa au kudharauliwa
vi. Itikadi na maadili/utamaduni: tofauti katika itikadi na utamaduni zisipochukuliwa vizuri huwezi kusababisha migogoro
Jinsi ya kuchambua vyanzo vya migogoro
Kuna mambo makubwa mitatu ya kuangalia wakati wa kuchambua migogoro:
i. WATU: ni akina nani wanahusika katika migogoro huu, wanahusikaje na nini mchango wao katika migogoro huu?
ii. MCHAKATO: hapa tunaangalia historia ya migogoro wenyewe. Je kuna utaratibu uliokiukwa au kusahaulika ambao ndio umesababisha migogoro> kwa mfano ardhi ya kijiji inapouzwa bila huhusisha wanakijiji mara nyingi huleta ngogoro baadae
iii. TATIZO: watu wanaozozana wanagombania nini? Nini KIINI cha mgogoro huu
Je unahisi kwanini migogoro mingi hujirudia rudia? Comment below
No comments
Post a Comment