Kitumwa
Hawa wamefundishwa woga na roho mbaya, mara nyingi wazazi wamewafundisha kuwa watii wakiwa na watu wakubwa. Wakitafsiri kwamba chochote watakachokifanya kitatafsisira kuwa ni utovu wa nidhamu na huenda wakapata adhabu.
Wamefundishwa na wanaamini kuwa watu wote walifanikiwa wametumia njia haramu kufika hapo walipo kama vile wizi, uchawi na kadhalika. Pia wanaamini kuwa endapo akija kiongozi wanapaswa kumwambia shida zao ili wasaidiwe na wanajua kuwa tajiri anapaswa kuibiwa.
Tabia unazowajengea
a) Kulalamika
b) Kuomba hata kama wanaweza wanachokiomba
Kawaida
Hawa wamefundishwa kuwa polepole, hakuna haja ya kufanya haraka kwenye maisha, soma utakuja kufanikiwa tu. Bandu bandu humaliza gogo, simba mwenda pole ndiye mla nyama.
Hawa huamini kuwa wakiwa na taaluma ndio kufanikiwa wao, hujua kuwa kuna taaluma bora kuliko zingine kwahiyo huwaambia watoto wao wasome ili waje wawe madaktari, waandisi na marubani
Tabia unazowajengea
a) Maringo dharau sababu wana nafasi kwenye jamii
b) Hujitofautisha na wengine sababu hujiona bora
c) Walalamishi kwa mabosi wao
ii Kifalme
Hawa hufundishwa mambo muhimu kwenye maisha yao, hufunishwa misingi ya kibinadamu zaidi ya taaluma. Hufundishwa Itifaki, heshima na nidhamu, kufanya kitu kwa wakati na mahali pake. katika umri mdogo huwa wanasoma mambo yanayowahusu na sio elimu ambayo kila mtu anayo
Huwa na maamuzi toka wakiwa na umri mdogo na wazazi hawawaadhibu wanapokosea ila huwaonyesha madhara ya makosa yao, hapa kinachoadhibiwa na tabia na sio mtoto. Mlishawahi ona watu ambao wakitoka Shuleni huenda dukani kwa wazazi wao.
Tabia unazowajengea
a) Heshima
b) Kuskiliza
c) Wapole kwa muonekano sababu hawaruhusiwi kulalamika
d) Huwa buzy wakati wote
Kwa tabia zao huwa wanaaminika na kutawala wengine sababu wanaonekana kuwa wanawajali na kuthamini watu wengine ulishawahi sikia “mbona boss mwenyewe hayuko hivi?” boss anajua jinsi ya kuishi na nyie ndio maana mnamwamini na kumfanyia kazi
Chagua njia bora ya kumle mwanao
No comments
Post a Comment