MALEZI YA WATU MASHUHURI



Jifunze kitu toka kwa hawa:

Daudi

Ni mfalme wa pili wa Israel, alikuwa mchunga kondoo na hata wakati Samweli anakuja kumpaka mafuta nyumbani kwa baba yake hakuitwa. Labda alionekana hawezi, au ana kazi yake na hapaswi kuwa na kazi nyingine.

Katika kazi yake ya uchungaji wa kondoo ilimpa ujasiri na yeye ndiye mfalme ambaye alipigana vita nyingi kuliko wafamle wote wa Israel. Alianzia kumpiga Dubu na simba alipokuwa anataka kumdhuru kondoo. Akapanda na kumpiga Goliati na alipokuwa na umri wa miaka 23 tu aliweza kuwa mfalme juu ya baadhi ya makabili ya Israel na alipokuwa na miaka 30 aliweza kuwa mfalme juu ya Israel yotee

Hakufundishwa mambo mengi hivyo alikuwa mtu wa kukosea sana kwaajili ya unyenyekevu wake alijirudi mara nyingi na kitabu chake cha Zaburi kimejaa msamaha na maombi mengi

 

Suleiman

Alilelewa kwenye nyumba ya mfalme hivyo alifundishwa vitu vingi vya Kifalme ikiwemo

·         Itifaki 1 Falme 3:7 “Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia

·         Uongozi

·         Sala na ibada

·         Kufanya biashara

Kwa hayo yote aliweza kuwa mfalme ambaye aliweza kuongoza nchi bila vita na nchi ilifanikiwa sanaaaa

 

Alexander the great 


 

Alipokuwa na miaka 10 aliwekewa walimu mashuuri ili kumwandaa kuwa kiongozi

  1.                   Generali wa jeshi: huyu alimfundisha kuhusu taratibu za kijeshi na nani wa kumwamini na asiye wa kumwamini. Mbinu zote za kivita najunsi ya kupigana
  2. Mwalimu wa Ithaki: alimfundisha taratibu za Kifalme, nini cha kufanya wapi, muda na kifanyejwe. Pia alimfundisha wapi amkanyage mtu na wapi asimkanyage na vyote vitakuwa na madhara gani
  3.  Mwalimu wa sayansi: alimfundisha alimu ya science ya darasani
  4. Aristotle: alimfundisha kinsi ya kufanya maamuzi. Na mshahara wa Aristotle ulikuwa ni kijiji chao kilijengewa nyumba za kufahari

Alifundishwa ndani ya miaka 3. Siku moja alimwona farasi mmoja mkorofi aliyekuwa hataki kufundishwa, akamwomba yule farasi, aliweza kumtuliza na kutembea nae bila kusumbua. Baba yake alipoona vile alimwambia, “Macedonia ni ndogo sana kako tafuta ufamle ukatawale”

Alipokuwa na umri wa miaka 20 ufalme wa baba yake ulitekwa na kupinduliwa, yeye aliweza kupigana na kutwaa ufalme tena kisha aliendelea kuteka famle nyingine kubwa Ulaya na sehemu za Asai alikufa akiwa na miaka 30 lakini ni mmoja kati ya wafalme watatu wenye nguvu zaidi waliowahi kutawala

 

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo