Katika hatua mbali mbali za maisha kila mtu ana mwalimu wake. Nikisema ujifunze kumuheshimu mwalimu wako ni kwa sababu
a. Mwalimu ana elimu ambayo ndio inayomfanya awe mwalimu na wewe ni mwanafunzi
b. Mwalimu anajua ukitoka hapo unaenda wapi kwa hiyo anaweza kukuunganisha na maisha baada ya hapo
Sasa basi kuna vitu ambavyo wakati mwalimu anakufundisha kuna wakati huwa hakufundishi kinachomfanya awe mwalimu labda geography au civics ila anaanza kukufundisha kuhusu maisha tu. Hiyo ndio hulka ya mwalimu
Sasa wewe ni mwanafunzi unaadhibiwa alafu unaamua kwenda kumsemea mwalimu kwa mzazi wako, unamwambia mzazi wako maneno ya uchonanishi unampanga mbaka unajua mzazi japanika. Kesho yake mzazi wako anakuja kumvaa mwalimu kwa maneno yasio na heshima tena mbele ya walimu wengine unadhani mwalimu atakufunzisha kitu kingine tena kukusaidina au atakuwa anakuja darasani kukufundisha Physiscs na kugeuza na kuondoka?
Mwalimu atasema ngoja nisimsemeshe huyu mwanafunzi kitu tena. Hapo jua hata akikuona unapotea atakuacha akiilinda heshima yake. Na wewe usipotaka kurekebishwa jua huna unapoelekea na hakika utaanuka. Waebrania 12:7-8 BHN inasema “Vumilieni adhabu kwani ni mafundisho; Mungu huwatendea nyinyi kama wanawe. Maana ni mwana gani asiyeadhibiwa na baba yake? Lakini msipoadhibiwa kama wana wengine, basi, nyinyi si wanawe, bali ni wana haramu.”
Walimu wanachokitaka ni kitu kimoja tu ambacho ni HESHIMA ili uweze kufaidi hekima na uzoefu walio nao. Nitakupa sababu:
Walimu wameona mengi kwa umri tu ambao wamepishana na wanafunzi kwa harakaharaka tu kwam mwalimu aliemaliza chuo akaja moja kwa moja kazini amepishana na mwanafunzi wa form four miaka 6 ukizunumzia uliemkuta Shuleni na anafundisha kwa miaka 10 amekuzidi miaka zaidi ya 15. Hivyo basi ameona mengi ambayo anaona unayafanya na hataki yakutokee wewe. Kaona kwa wanafunzi wengine, mtaani, hadithi za mtaani n.k
Waheshimuni walimu wenu mjifunze mengi, Yesu alikaa na wanafunzi wake kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita akawaamini akawapa ulimwengu wewe nikikuuliza: baada ya mwalimu wako kukaa nawe miaka 4 anaweza kukuamini hata awe referee kwente CV yako?
No comments
Post a Comment