Yusufu: Simamia ndoto zako
Yusufu alikuwa mwota ndoto, aliota ndoto ambazo wenzake hawakuzipenda ila yeye aliziamini licha ya kuwa alijua alichukiwa na ndugu zake lakini hakuwachukia ndugu Mwanzo 45:4 Yusufu akawaambia ndugu zake “karibuni kwangu” basi wakakaribia. Akasema, “Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri”
Aliamini kuwa ilikuwa njia sahihi.Mwanzo 45:5 “basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu”
Yusufu Alipitia:
· Kuuzwa na ndugu zake
· Kuwa mtumwa
· kusingiziwa kubaka
· Kufungwa
· Kuwa waziri mkuu wa Misri
Mungu haumwonyesha hayo yote maana kama angejua atakayopitia asingetaka kwenda hivyo kupishana na lengo la Mungu
Usimzuie mwanao kupitia changamoto maana haujui ni nini kilichopo mbele yake unaweza kuwa wewe ndio chanzo cha kuzuia baraka zake
Daniel
Alichukuliwa kwenda utumwani akiwa na miaka kama 18 hivi. Alipokuwa utumwani hakuacha utaratibu wake wa ibada. Daniel alikuwa akiomba mara tatu kwa siku akifungua dirisha kuelekea Yerusalem
Alifanywa kuwa mshauri wa mfalme sababu ya hekima iliyoonekana ndani yake ila alionekana tena kuwa eneo la ushauri halimtoshi na kuwa waziri, pia uwaziri haumtoshi akafanywa kuwa waziri mkuu katika nchi ya utumwa. Yaani alipelekwa kutumikishwa akaenda kutawala
Daniel ndiye kiongozi ambaye alikaa kwenye uongozi kwa muda mrefu sana maana aliongoza kwa miaka 70
· Mfundishe mwanao kusali na kuomba.
· Mwambie kuomba ni sirini na kusali ni mbele za watu.
· Mwambie ashukuru kupata chakula hata kama anakiona kiko stoo
· Mwambie ashukuru sababu pumzi aliyo nayo ni kwa neema tu
· Mwambie maombi yatamsaidia sehemu ambayo hakuna atakaeweza kumsaidia
· Mwambie hata kama haupo maombi ndio masingi wa kila kitu
· Mwambie aombe Ufalme wa Mungu ndani yake
· Sali nae apate mfano toka kwako
Msisitize kuwa asidharau maombi, yanabadilisha mambo, hali na vitu
No comments
Post a Comment