1.
Shauku
Isikilize sauti ilioko ndani yako, ambayo inakuambia Unachotakiwa kufanya ni sauti ya upole na inakuonyesha ukiwa unafanya kitu tena unaskia raha sana ukiwa kwenye hayo mawazo. Huyo ndio wewe ukifanya hicho kitu utafanikiwa sana, acha mambo ya kuiga sijui udakitari upailoti ili uonekane na wewe unamalengo makubwa
2. Andika unachotaka kufanya
Kuandika kunakupa kukumbuka kitu unachokitaka na unachotaka kufanya. Andika unachotaka kufanya hata siku ukisahanu utaweza kukumbuka kila kitu ukisema ulipo Andika
· Andika unachotaka kufanya maishani
· Andika ambacho hutaki maishani mwako
· Andika unavyojiskia
3. Weka malengo 3
Weka mambo mitatu ambayo utayafanya kila siku na kuyakamilisha. Weka jambo moja utakalofanya kila siku kwenye:
· Kiuchumi kama ni kusoma, kuwekeza au kuweka akiba
· Mwilini mfano mazoezi
· Lengo kila mtu ana leno lake la wito au mahali alipo. Kama upo chuo lengo ni kusoma, kama uko kazini fanya kitu cha tofauti kila siku kufanya kazi yako kuwa bora
Haya mambo mitatu yatatumika kama ramani ya unakokwenda
4. Plan
Kuwa na malengo ukiwa na malengoutakuwa na mipango ya muda mrefu na mfupi
· Tafuta njia utakayoitumia kufikia malengo yako ya muda mrefu
· Weka mipango ya muda mfupi ukiyaweka kwenye muda maalumu (hakikisha unatimiza ) na kufanya marekebisho pale inapohitajika
· Rudia mpaka utakapotimiza malengo yako
5. Tatua changamoto
Kama unahitajikufanya mabadiliko lazima ubadilishe system nzima lazima kuwe na mabadiliko ya lazima kiakili na kimwili nakushauri Tatua changamoto zako kila siku kidogo kidogo baada ya muda utakuwa mtu bora zaidi
6. Fuata shauku
Shauku ni kile kitu ambacho unatamani kukifanya na ukiwa unakifikiria ama kukiwaza huwa unajiskia Amani sana moyoni. Inawezekana sio udaktari, urubani n.k. inawezekana ni kitu ambacho ukikisema kwa watu waliokuzunguka watakushangaa inawezekana ni upishi, ucheshi nk. Kianze tu kwa udogo wake baada ya muda kidogo utakuwa mtu mkubwa na waliokucheka watakuja kutafuta kazi kwako. Upishi unaweza kuwa hoteli, ucheshi unaweza kuwa WatuBaki usijidharau
7. Jifunze bila kuchoka
Ili usipoteze muda katika maisha yako jifunze bila kuchoka ili uweze kujifunza fanya hivi:
· Jidhibiti nafsi yako: utaweza kudeal na matatizo yako kwa asilimia 70 kama tu ukiweza kujidhibiti nafsi yako
· Soma zaidi ili kusaidia wengine
8. Tatua Matatizo yako na tafuta wito wako
Ili kushughulikia matatizo yako
· Toka kwenye njia ambayo unayoona ni mbaya na haiendi kokote, hii njia unaijua ukiingia”toka huko”
· Pambana na mwili wako uwe silaha ya kazi Ili kujibadilisha na kuwa mtu wa tofauti
· Badilisha mtazamo wako
· Jipangie vitu vya kufanya kila siku ambavyo vitashughulisha akili na mwili
No comments
Post a Comment