VITU MUHIMU KUMFUNDISHA MWANAO

 


Kuna vitu vya msingi sana tunakosa kwa kizazi cha sasa hivi, ambavyo ndio maisha yetu ya kila siku. Sisi tumebakia kwenye kila mtu kuwa na taaluma lakini hatujui kuwa kuna zaidi ya taaluma. Kwasababu tumeweka juhudi zaidi kwenye taaluma na kusahau mengine imetufanya tumekuwa kinyume na taaluma zetu. Mfano askari ndio wamebadilika na kuwa wahalifu, walimu ndio wanaodananya, vionozi wa dini ndio ambao hawaamini wanachotufundisha hizi ni baadhi tu ya vitu vya msingi vya kumfundisha mwanao.

        Uaminifu

Mfundishe mwanao Uaminifu kama vile, asichukue kitu ambacho sio chake, atoe taarifa ya kitu kilichopotea. Uaminifu wa kazi yaani akiambiwa kitu kufanya afanye ndani ya muda na sio vinginevyo. Baadae ataweza kuaminika kokote ulimwenguni

 

      Kuskikiza zaidi ya kuongea

·         Mwambie asikilize zaidi kuliko kuongea

·         Kwambie ana masikio mawili na mdomo mmoja

·         Mwambie viongozi wote wanaskiliza zaidi kuliko kuongea

·         Mwambie hata ukimya ni jibu

Baba yake Mandela alikuwa akienda kwenye kikao alikuwa anawaskiliza watu yote kabla ya yeye kuongea na hapo kilimfanya kuwa kiongozi bora na ndipo Mandela alipojifunzia uongozi

 

Hata kama sio kiongozi mwambie ajifunze jinsi ya kuwasiliana  nakatika kuwasiliana kuna kuskiliza zaidi kuliko kuongea na ataweza fanikisha kilakitu anachotaka kufanikisha.

·         Mwambie Malumbano hayajengi

·         Hatafutwi msindi ila anachotaka ahakikishe kimefanyika

        Kutunza siri

Sio kila kitu cha kweli kinapaswa kusemwa na sio kila kosa ni kosa, mfundishe mwanao awe na kifua cha kutunza siri na sio kila anachokiona anataka kuwa wakwanza kukisema. Ulishawahi kuona wale ambao wanafowadi meseji kwenye magroup ya whatsapp akafu wanakuta hicho kitu kilishatumwa masaa mawili yaliotipa?

 

Wafundishe wanao wakona kitu waangalie mambo haya kabla ya kukisema

·         Uhusiano

·         Muda

·         Nguvu alizo nazo au walizo nazo juu ya hali halisi

·         Umri

Maana wanaweza toa siri wakaharibu zaidi badala ya kujenga

        Nidhamu na sio utii

Nidhamu ni uwezo wa kufanya jambo linalopaswa mbele ya watu na hata kama watu hawapo bado utafanya. Utii ni kufanya sahihi mbele za watu na wawapo wenyewe hawajali lolote. Ulishawahi waona watu ambao wakiwa mbele ya boss wanafanya kazi sana lakini boss akiondoka hakuna wanalofanya?

 

Nidhamu itamjengea Uaminifu maana kila mtu atamwamini kumpa kazi zake akiamini hata asipokuwa nae atafanya. Watu hawa wanajituma kwa Uaminifu.

      Itifaki

Watoto wako wajue nini cha kufanya, wakati wa kufanya na namna ya kufanya. Nani wa kuongea nae na namna ya kuongea nae

Wanao wajue

·         Kumpisha mtu mzima apite kwanza

·         Akiongea na mtu mzima avue kofia

·         Amjibu mtu mzima kwa nidhamu

·         Wakimwona mama mjamzito, mwenye mtoto, ama mzee kwenye gari wasimame akae

·         Wasalimie wakubwa na wadogo

·         Wawasaidie wasio jiweza kama maskini, yatima, wajane

 

Huo ndio utu

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo