Watu wazima wanapaswa kujitafakari sana pale ambapo wanawaadhibu watoto walati wao waliyafanya wakiwa na umri wa shule na endapo wangekamatwa makosa mengine wangefukuzwa shule. Hakuna kipya kwa watoto
Haya ni baadhi ya matendo ya watu
wazima waliyoyafanya wakiwa Shuleni
- Nilikuwa nauza chapatti bwenini
- Nilishawahi kuingia na simu Shuleni
- Kuagiza chips kwa njia ya magendo
- Nilishawarudisha mwenzangu waliokuwa wanadaiwa ada
- Nilishawahi sambaza uongo kuwa mwenzangu amekufa
- Nisishahusika kwenye kumkamua ng’ombe wa mkuu wa shule nikaenda kuuza maziwa mtaani
- Nilishamkamata kuku wa matroni tukamchinja na kumla
- Nilipokuwa form four wakati wa mitihani niliiba chakula cha wanafunzi
- Tulishawahi iba cement ya shule tukapeleka dukani tukapata mkate
- Nilikuwa nauza karanga wakati mwalimu anafundisha
- Nilikuwa stoo ya vitabu nikawa nauza madaftari kwa wenzangu
- Siku moja niliamua kulala bwenini wakati nilikuwa mwanafunzi wa day
- Tulimfunika mwalimu alipokuwa amesinzia darasani
- Niliiba chakula cha walimu na walimu wengine wakakosa
No comments
Post a Comment