Kutokuwa na lengo la ndoa
Watu wengi wanaingia kwenye ndoa pasipokuwa na lengo la kuingia kwenye ndoa, mfano watu wanaingia kwenye ndoa wakiwa na lengo la kulea watoto na inapofika kwenye utu uzima hawana lengo tena la kukaa wawili. Unapaswa kuwa na lengo kubwa zaidi ya hilo ukiwa unaingia kwenye ndoa
Kuangalia mambo ya kimwili
Jambo lingine ni watu wanaingia kwenye ndoa sababu maumbile ya mwili, mfano uzuri wa mwanamke au mwanaume na endapo mmoja wapo atabadilika kwa sababu yeyote ile ikiwemo uzazi basi patner wake atatafuta mtu mwingine atakaekuwa anafanana na anachokitaka.
Uchumi
Watu wengine wanaingia kwenye ndoa sababu wanataka msaada wa kiuchumi, wakitegemea kuwa mume/mke atamsaidia kiuchumi au atafanya lolote nyumbani kwao. Endapo akijiweza na kuweza kujitegemea kiuchumi anaona hakuna haja ya kuwa pamoja
Ndoa nyingi zimevujika japo watu wengi wanaishi pamoja, wako kimwili ila roho zao ziko mbali, sababu ya wao kuishi pamoja ni kuonekana wanaishi pamoja kwa watoto. Sababu zinzofanya watu kuishi pamoja mioyo kuwa mbali ni pamoja na kutosamehe na Kutojali hisia za mwenzako
No comments
Post a Comment