Kuwaambia tu kile ambacho si sahihi:
Kufanya kwa kumwambia mtoto mambo ambayo
hawatakiwi kufanya kunawafanya wasikie makosa tu na hicho ndicho
watakachokifanya maana ndio wanachosikia
Kufanya makosa wakati tunawarudi:
Mfano motto amekuja kukushitakia kuwa mwenzake kampiga wewe unamwita mwenzke na kumwambia “ we mpumbavu kwanini umempiga mwenzako?” hapo ni kuwa, mtoto kampiga mwenzako na wewe umemtukana mtoto
Kukemea matendo yasiyohitajika:
sisi katika
kukuza watoto tuna vitu vingi sana ambavyo ni “usifanuye……..” hatuwaambii
watoto wanachotakiwa kufanya. Kwa sababau hawana wanachotakiwa kufanya hujikuta
wakiwa wanafanya walichoambiwa wasifanye
Kuwafanya watoto wafuate sharia kwa kuweka vitisho vya adhabu:
Watoto siku zote watatafuta njia za kukimbia adhabu hata ukiwa unawarudi hawatasema kitu kama hujatumia njia ambayo ni sahihi
Kutokujihusisha na mabo ya watoto kwa ukaribu kwa kuwa walishasomewa sheria:
Usichukulie kuwasomea sharia kuwa ndio umemaliza, kwa akili za watoto hata huwa hawakumbuki kwasababu wamesomewa ila wakizitunga hilo ni swala la tofauti
Kuwakemea na kudhuru mwiliwakati wa kuwarudi
Kuwaadhibu na kuwakemea pale wanapowakosea wengine bila kujali usuluhishi:
Mfano,mtoto anakushtakia mwenzane alafu umamwita mwingine na kumchapa lisha maisha yanaendelea hilo ni kosa
Kutokutambua na kutoendeleza vipaji vyao:
Kutokujali tabia za watu wazima wanaowahudumia watoto kama kioo ambacho watoto hujiangalia
Kuwaadhibu watoto wanapofanya makosa bila kuwasaidia kuyaelewa vizuri
makosa yao na Athari zake
Kuwaunganisha watoto na tabia zao na kuwapa majina mabaya mf mwizi