Aliyetoga mwili wake
Mara nyingi mwanamke aliyejitoboa sana mwili wake kuwa ni mkorofi, asiyejali pia ni mtu ambae anaingia gharama nyingi zisizo na sababu na mara nyingi hana heshima na kuwa na mahusiano na watu wengi
Mwenye tattoos
Tattoo ni utambulisho wa kitu pia ni utambulisho wa mtu kuwa anajihusisha na kundi fulani la siri hii ni kama anajua au hajui. Pia mazingira mtu huyo hufikia na kuchora tattoo huwa ni mazingira ya kihuni sana. Sasa fikiria umempata mwanamke ambae ana tattoo na kukwambia haina shida my friend huna mtu hapo. Ila endapo una uhakika na mazingira ya mtu husika kubadilika unaweza kumwamini. Watu hubadilika
Mwenye marafiki wengi wa kiume
Mwanamke mwenye company kubwa ya wanaume sio wa kumwamini maana huwezi jua kwa uhakika kama ni marafiki au kuna ambaye ana uhusuao nao, hawa mkizunguana tu hana baya anakubadilisha tu chap na kuwa na mtu mengine kwenye group lake. Sio vibaya kuwa na marafiki wa kiume ila wasiwe ndio company yako kila uendapo
Mwenye matatizo na baba yake
Lazima mtu awe na uhusiano mzuri na baba yake ili aweze kuishi na wewe, kama ana matatizo na baba yake basi atakuwa na matatizo na wewe pia. Wanawake wengi ambao walioshuhudia mama zao wanaishi bila kuwa na baba yake hawaoni umuhimu wowote wa kuwa na mume wao pia, so ukiwa nao jua kutakuwa na issue na wewe. Naomba kueleweka hapa kuna tofauti kati ya mwanamke ambae alimwona baba yake akiwa mbali au aliyefariki na yule ambae hakuonyeshwa baba yake huku anafundishwa kuwa “baba yako ni mjinga”
Matumizi ya kupindukia ya mitandao
Wanawake wengi ambao wanahangaika sana na social media huwa hawajali mambo mengi ya msingi, Matumizi ya kupindukia ya mitandao ya kijamii imehusishwa na matatizo kadhaa ya afya ya akili, ikiwa ni pamoja na wasiwasi, unyogovu, na upweke. Mitandao ya kijamii inaweza husababisha mtu kuwa na matarajio yasiyo ya kweli kuhusu muonekano, mahusiano, na mafanikio, hawa ndio ukiwauliza wanataka kuja kuwa nani watakuambia vitu vya kusadikika mpaka unashangaa
Mwenye mahusiano na watu wengi
Hii maana yake ni mtu ambaye amekuwa na wapenzi wengi ogopa sana mtu huyo sababu wana:
i. Wivu au kutojiamini,
ii. Matarajio tofauti,
iii. Mitazamo tofauti kuhusu Uaminifu
Hawa hawana wanakoenda achana nao
Anaeangalia anapata nini toka kwako
Hawa hupuuzia vitu vyote vya msingi endapo hawajapewa mahitaji yao, yaani wape pesa ndio wafanye menginge huitwa gold diggers au slay queens. Ili waendelee kuwa na wewe lazima uwape wanachokihitaji na kila wakati mambo hayaendi kama unavyopanga wakati mwingine mambo huyumba na wakati yatapoyumba hawa hawana muda na wewe wanaenda kutafuta mtu mwingine, hawa hawana kokote wanakoenda kama wewe una uendapo basi achana na hawa
Walevi na waenda night club
Hawa wanapenda kila wakati kwenda kwenye parties, wanapenda kwenda club, wao kila weekend wao lazima watoke, matumizi yao ya pesa mara nyingi ni parties navinywaji. Ukikutana na msichana anasema anavuta shisha tafuta njia ya kuondokea ukimwona anakunywa pombe sana hebu usiongee neon lingine na anaependa parties jifunze kusema HAPANA
No comments
Post a Comment