Maana ya migogoro:
Ni hali ya kutoelewana kati ya mtu na mtu au kundi moja na jingine, ambayo hutokea wakati shughulia ya pande mmoja inapozuia au kuingiliana na shughuli ya upande mwingine
Migogoro pia ni kutofautiana kwa mtazamo wa maoni kati ya pande mbili kuhusu jambo fulani. Migogoro ni sehemu ya maisha ya binadamu na pia migogoro huwezi kuwa chanzo cha mabadiliko chanya
Aina za migogoro
i. Migogoro iliyojificha na kuendelea ndani kwa ndani (covert conflicts)
ii. Migogoro iliyojitokeza wazi (overt conflicts)
Mitazamo kuhusu migogoro
Watu huwa na mitazamo tofauti kuhusu migogoro
a. Traditional view: hawa huwaamini kuwa migogoro ni kitu kibaya na hivyo ni wa kuepuka kwa gharama yeyote. Watu wenye mtazamo huu hawapendi kukosolewa, pia ni wagumu kupokea ushauri. Huchagua marafiki ambao hawapingani nao. Wanapojikuta kwenye migogoro kupata ‘stress’ na kutoa vitisho kwa wale wanao tofautiana nao
b. Behavioral view: hawa huamini kuwa migogoro haiwezi kuepukika watu wanapoishi pamoja. Watu hawa wapo tayari kukosolewa na kupokea mawazo tofauti, kwa sababu wanajua kwamba binadamu hawafanani katika kufukiri. Wana uwezo wa kupokea migogoro bila stress na wanaweza kuchananyika na watu wa kila aina
c. Interactional view: watu wenye mtazamo huu huamini kwamba migogoro ni sehemu ya uhusianao wa kibinadamu na mara nyingi huchochea mabadiliko chanya. Wanaamini kwamba migogoro huleta mawazo mbadala na hivyo wanaweza kujifunza mambo mazuri kupitia migogoro
Je wewe una mtazamo gani kuhusu migogoro? Comment hapo chini
No comments
Post a Comment