KUJITUMA KUNALIPA


Hadithi ya kelvin

Kelvin alizaliwa kijiji cha  Benji iliyoko wilayani Hai Kilimanjaro, alipokuwa darasa la tano baba na mama yake waliachana na Kelvin alibaki na baba yake ambae alimwamishia shule ya bweni kwasababu baba yake ni dereva wa magari ya mizigo, hivyo hashindi nyumbani mara nyingi. Kelvin ni mwanafunzi wa wastani darasani ila anajitahidi ili afaulu maana baba yake alimwambia kuwa huo ndio urithi wake

Alipomaliza darasa la saba alienda shule ya sekondari, siku moja baba yake alimtembelea na kuongea nae akimtaka aongeze juhudi katika masomo yake. Kelvin aliamua kuchukua hatua na kusoma kwa bidii, alianza kuamka usiku na kusoma muda wa ziada, siku za mwisho wa wiki hakuwa anaenda kucheza mpira muda mrefu ila alitumia muda mwingi kujisomea

Alipofika kidato cha pili walifanya mitihani wa mock kelvin alikuwa mwanafunzi bora kwenye somo la kemia na hiyo ilimpa moyo kuwa juhudi zake zinazaa matunda, licha ya kupokea zawadi pia yeye ndiye mwanafunzi anayeongoza darasani

Walipofika kidato cha nne pia walifanya mitihani wa mock na kelvin alikuwa mwanafunzi aliyeongoza katika somo la physics licha ya kuwakatika wilaya ya Hai kulikuwa na wanafunzi wenzake waliokuwa wanaongoza alipokuwa shule ya msingi

Aliemaliza form four kwa kupata daraja la kwanza na kupangiwa shule ya Songea boys kwenye combination ya PCB na aliemaliza shule kwa daraja la kwanza. Chuo alipangiwa Herbert Karuiki University ambapa anachukua masomo uake ya udaktari

 

The story has been inspired by true story

 

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by templateszoo