NJIA 6 ZA KUIMARISHA UFANISI WA KUJITAMBUA
a. Uliza Maoni:
- Tafuta maoni kutoka kwa wenzako, marafiki, au wafanyakazi. Hii itakusaidia kutambua na kurekebisha maoni yasiyo sahihi uliyonayo kuhusu nafsi yako. Kuuliza maoni juu ya mambo mbalimbali kutaweza kukuimarisha kwa kujirekebisha
b. Tambua uwezo na Udhaifu Wako:
- Hii itakuruhusu kudumisha uwezo wako na kufanya kazi kwa bidii kuboresha udhaifu wako.
- Kwa kufahamu udhaifu wako kutakupa nafasi ya kujikaua na kujirekebisha kila mara.
- Ukiweza kuzifahamu sehemu ambazo uko imara mfano kufanya kazi kwa bidii, ufanisi wa mambo mbalimbali kutasaidia sana kukabiliana na udhaifu wako kama ukiendelea kujibidisha zaidi huki
c. Jiangalie Kwa Kina:
- Kujiangalia kwa kina kunaweza kufungua mawazo na hisia ambazo huenda zingeachwa bila kutiliwa maanani.
- Njia bora ya kujiangalia kwa kina ni ile ambayo kila ukimaliza kazi unaangalia wapi ulipokosea na wapi ulifanya vizuri. Mfano Ukipokea mitihani na ukaona huna alama za kutosha usiutupe, bali uangalie wapi ulijibu kimakosa ili wakati mwingine usikosee kosa lilelile
d. Fuatilia Mawazo Yako Binafsi:
- Mara nyini mawazo yenye nguvu hutoka ndani mwa mtu na sio nje. Nikisema ndani namaanisha “mawazo” na nikisema nje namaanisha kwa kusikia au kuona watu wengine wanasema nini
- Ni vizuri kufata mtazamo wako hasa kwenye swala la maamuzi na endapo utakuwa na wasiwasi tafuta mtu mzima alafu umwambie kisa chote kisha akushauri, chukua unayoyaona yanafaa zaidi na sio kuchukua ushauri na kuacha mtazamo wako
e. Jifunze Kusema "HAPANA":
- Kusema “HAPANA” sio kosa hasa pale unaposhirikishwa swala ambalo unajua fika sio sahihi au ni sahihi lakini sio wakati sahihi
- Kusema hapana haimaanishi kuwa wewe ni mshamba
- Kama unajua unakoenda na umejiwekea malengo yako ya unakoenda, jua kuwa na kiasi na usisite kusema “HAPANA” inaweza kukufanya ukagombana na watu ila pia inakupa uhakika wa kufikia malengo yako ya muda mrefu
f. Uliza Maswali Kuhusu Maamuzi Yako:
- Hakikisha kuwa maamuzi yoyote unayofanya ni sahihi kwa kuuliza maswali na kuweka misingi kwa kutoa sababu tatu za kufuata njia fulani. Mfano lengo ni kufaulu mitihani weka sababu tatu kwanini unataka kufaulu mtihani Hii itakusaidia kuelewa vizuri lengo lako na kuwa na uhakika kuwa umechagua chaguo sahihi
Kuwa na uwezo wa kujitambua ni muhimu katika safari ya maendeleo ya mtu kibinafsi. Kwa kutumia njia hizi, unaweza kuimarisha uelewa wako binafsi na kujenga msingi imara wa kukua na kufanikiwa.
No comments
Post a Comment