1.
Kuchanganyikiwa
“Sijui cha kufanya”
Ukifikia hapa unachoka na mawazo mengi sana. Andika mawazo yoteambayo yako kichwani alafu anza kuchambua moja moja kwa kuangaliafaida zake na hasara kisha chagua njia ambayo inakufaa. Anza kidogo ukiwa na kitu cha kuanzia na ukakosa uamuzi, ni kwasababu una machaguo mengi, chagua moja hiyo pia ni njia ya kutokea na utafika
2. Hofu
“Siwezi”
Ukisema huwezi uko sahihi, na ukisema unaweza uko sahihi pia, ila shagua mtazamo ambao utakusaidia kufikia malengo yako
Usiogope kitu chochote kwa lolote lililoko moyoni lina sehemu ya kuanzia na ukianza tu njia iko wazi mbele yako. Maisha yako kama mtu anayeendesha gari usiku anapowasha taa taa zinamulika mita chache tu kila anapoendelea kuendesha ndio mwanga wa taa unaposogea mbele na kuona mita chache za mbele. Asipoendesha atabaki kuona sehemu moja akianza tu njia inafunguka. Acha woga fanya jambo
3. Mtazamo usiobadilika (fixed mindset)
“Itakuwaje nikifeli”
Vipi sasa kama ukifanya alafu ukafanikiwa. Ukijiwekea mtazamo mmoja tu ambao ni kufeli utashindwa kwenye kuchukua hatua. Kufeli ni ada ya kulipia kwenye somo la maisha huwezi fundishwa bure, na kama hutaki kulipa ada hakuna mwalimu atakaekufundisha
4. Ulegevu
“Nimechoooka”
Hii sentensi huwa inakunyima kufanya mambo mengi, Unachotakiwa kufanya ni kukifanya kile ambacho unaona kinashindikana ukiendelea kutoa sababu hiyo hutakaa ufanye kitu. Ili kuishinda hiyo hali basi basilisha muda ambao unataka kufanya vitu vyako ili kukamilisha mambo yako
5. Kutojali
“Sijali lolote”
Ulishawaskia watu wakisema hayo maneno? Alafu hawafanyi kitu sasa. Wananjiita bad boys au bad girls.
Kila mtu ana kitu ambacho anakijali, kinachofanya useme maneno kama hayo ni kuwa unahisi huwezi kufanya chochote tena. Tafuta kitu kimoja unachopenda na kujali na jitahidi kukifanyia kazi
6. Majuto
“Umri wangu umeenda siwezi kuanzisha kitu”
Muda sahihi wa kuotesha mti ulikuwa miaka 10 iliopita. Unawez kuotesha hata sasa na kula matunda yake. Usisikilize sauti yeyote inayokuambia huwezi kufanya hili wala lile, sababu ya umri au hali ulio nayo, maono hayo ulio nayo Mungu hakuyaweka moyoni kwa bahati mbaya, kuna makusudi kamili ya kukamilisha jambo hilo.
anza sasa
7. Utambulisho (identity)
Usijitsmbulishe kwa maneno yoyote mabaya “mimi ni mvivu”, “sielewagi” au “mimi ndivyo nilivyo”. Jua maneno yana nguvu na Mungu aliyatumia kuumba dunia hii na ikawa hivi. Ukiendelea kijisemea maneno mabaya yatatimia kwenye maisha yako. Jifunze kujitambulisha kwa utambulisho mzuri